Hitmaker wa ‘Nani Kama Mama’, Christian Bella amesema kama wasanii wakiendelea kukimbilia Afrika Kusini kwenda kufanya video zao, watakuwa maskini kutokana na gharama kubwa wanazotumia.
Akizungumza na kipindi cha Siz Kitaa hivi karibuni, Bella alisema ingawa muziki unalazimisha hali hiyo, wasanii wanatakiwa kuwa makini.
“Wasanii kukimbilia South Africa inaweza ikasababisha wasanii wafe na umaskini,” alisema. “Utachelewa kujenga, utachelewa kufanya mambo ya hela, unampelekea Godfather. Bongo tuna director wakali ila kinachotukwamisha ni connection ya MTV Base na TV nyingine kubwa,” aliongeza muimbaji huyo.
“Yaani tunaomba Mungu madirector wetu wapate connection ya kuufikisha muziki wetu kule mbele. Wakimaliza hali hiyo mimi si nammchukua Adam Juma kwenda kushoot video hata Dubai si najua itafika mbali? Tukiendelea kukimbilia South tutakuja kufa maskini.”
0 Response to "Christian Bella: Wasanii watakufa maskini wakiendelea kukimbilia South kufanya video"
Post a Comment